Jumatano 16 Aprili 2025 - 23:04
Kwa siku 44 hakuna maji, chakula wala dawa vilivyoingia Ghaza / Wanazuoni katika ulimwengu wa Kiislamu wako wapi?

Mwakilishi wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina alisema: “Kwa kipindi cha miezi 18 tumeshuhudia dhulma, mauaji ya halaiki, mauaji ya watoto, njaa na kiu huko Gaza. Kwa siku 44 hakuna maji, chakula wala dawa vilivyoingia Gaza. Ulimwengu huu si ulimwengu wa haki. Ni ulimwengu unaoendeshwa na kichaa kama Trump, na unaotetewa na Uzayuni wa kimataifa, huku viongozi wote wa nchi za Kiarabu wakikaa kimya mbele yake.”

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza: Nasir Abu Sharif, mwakilishi wa Jihad ya Kiislamu nchini Iran, usiku wa jana katika mkutano mkubwa wa wananchi wa “انا على العهد” (Mimi nipo katika ahadi) uliohudhuriwa na maelfu ya watu kutoka Iran na nchi nyingine Duniani, kwa lengo la kufanywa upya kiapo na dua ya kuomba msaada kwa Imam Mahdi (a.f) kwa ajili ya kuwaokoa watu wanyonge wa Ghaza na kuiangamiza serikali dhalimu na muuaji wa watoto ya Kizayuni, uliofanyika katika viwanja vitakatifu vya Msikiti wa Jamkaran, alisema: “Kutoka katika moyo wa Palestina, Ghaza na Msikiti wa Al-Aqsa nawasalimu ndugu zangu wa kiume na wa kike. Kuna uhusiano baina ya Imam Mahdi (aj) na Quds (Yerusalemu) ambao umetajwa katika riwaya, na uhusiano huo ni wa mapambano na upinzani wa Imam huyo dhidi ya Dajjali wa Kimarekani, Kiauroupa na Kizayuni.”

Akaendelea kusema: “Kwa kipindi cha miezi 18 tumeshuhudia dhulma, mauaji ya halaiki, mauaji ya kizazi, njaa na kiu huko Gaza. Kwa siku 44 hakuna maji, chakula wala dawa vilivyoingia Gaza. Ulimwengu huu si ulimwengu wa haki. Ni ulimwengu unaoendeshwa na kichaa kama Trump, na unaotetewa na uzayuni wa kimataifa, huku viongozi wote wa nchi za Kiarabu wakikaa kimya mbele yake.”

Mwakilishi wa Jihad ya Kiislamu alieleza kwamba: “Dunia katika kipindi hiki cha miezi 18 haijafanya lolote kwa ajili ya Ghaza, bali wengi wao wamewasaidia wazayuni katika jinai na uhalifu wao. Baadhi ya nchi za Kiarabu pia zimeisaidia serikali hii ya kihalifu. Katika hali hii, ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo iliyotoa msaada kwa Ghaza kwa mujibu wa malengo ya Imam Khomeini (ra) na miongozo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi. Vilevile, watu wa Yemen na Hizbullah ya Lebanon wamesimama bega kwa bega na watu wa Ghaza na wametoa gharama kubwa juu ya hilo.”

Mwakilishi huyo aliendelea kusema: “Wanazuoni wa ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu wanapaswa kuamka, kusimama na kukabiliana na miradi ya Kimagharibi na Kizayuni, kwa kuwa miradi hiyo si kwa lengo la kuiangamiza Palestina pekee, bali inalenga kuangamiza mataifa yote ya Kiislamu yanayopinga. Na tunashuhudia kuwa taasisi zote za utafiti za Kimagharibi zinaiona Uislamu kuwa ni adui wao na zinajitahidi kupambana na kila nembo ya Kiislamu.”

Akamalizia kwa kusisitiza: “Kwa sababu hiyo, sote tunapaswa kupigana na washirikina kwa mujibu wa amri ya Qur’ani, nasisitiza kuwa kama vile maadui wameungana dhidi yetu, nasi pia tunapaswa kuwa wamoja na wenye moyo mmoja dhidi yao na tupambane nao kwa nguvu zetu zote.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha